Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manesi 7 mbaroni kwa tuhuma za kuwauzia wagonjwa dawa

Dawa Za Nguvu Za Kiume.jpeg Manesi 7 mbaroni kwa tuhuma za kuwauzia wagonjwa dawa

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya wauguzi/manesi saba wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama wamefikishwa polisi baada ya kudaiwa kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane.

Wauguzi hao wanadaiwa kudakwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakiwa na dawa za aina mbalimbali kwenye pochi zao za mkononi (handbag).

Akizungumza nasi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba amesema wauguzi hao walikutwa na dawa mbalimbali ikiwamo drip za maji, dawa za kuongeza na nyingine.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipata malalamiko kutoka kwa wagonjwa kwamba wanauziwa dawa na manesi hao kutoka kwenye mikoba yao.

“Tulikuwa tunafanyia kazi hizi tuhuma hizo ambapo wenzetu wa Takukuru walifanya ukaguzi wa kushtukiza tarehe 24 Februari 2023 katika baadhi ya wodi na kawakuta wawakilishi wakiwa na dawa kwenye handbag zao.

“Waliwachukua na wakawahoji, baada ya kujiridhisha, nilienda hospitali nikakaa na uongozi na wafanyakazi na kuzungumza nao kwa kina.

“Nikawaagiza kutumia geti ambalo kila asubuhi msimamizi wa wodi alete taarifa ya utendaji kuhusu wodi husika kwamba mgonjwa kaandikiwa dawa gani na amezipata au lah ili haya masuala ya kuuziwa wodini yaishe,” amesema.

Amesema dawa hizo zinaweza kuleta madhara kwa wagonjwa kwani kwanza hawajui zimetoka wapi, pili haifahamiki ubora wake hivyo ni hatarishi kwa mgonjwa lakini pia hujuma hiyo inaikosema manispaa mapato.

“Ndio maana tukawapeleka polisi ili waendelee kuchunguzwa na kusearch-iwa, walichukuliwa maelezo na waliokidhi vigezo walidhaminiwa ila polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

“Uchunguzi ukikamilika tutapata mrejesho na hatua zitachukuliwa ikiwamo kupelekwa mahakama,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live