Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka yagawa Jiji la DSM katika Kanda hizi..

Bot.jpeg Mamlaka yagawa Jiji la DSM katika Kanda hizi..

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imeligawa jiji hilo katika kanda ‘vipande’ saba ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma zake karibu na wananchi. - Mkurugenzi wa jiji hilo, Jamaary Satura ambaye alianza kazi katika halmashauri hiyo Juni 17, mwaka huu, amesema kanda ya kwanza inahusisha kata za Kisutu, Kivukoni, Upanga Mashariki na Upanga Magharibi. - “Kwenye mikoa mingine utaona hili eneo la kata nne ni ukubwa wa halmashauri kabisa. Sasa utaona tukifanya hivyo maana yake ni kwamba wananchi wa kanda hiyo hawana sababu ya kuja kupanga foleni kubwa hapa halmashauri ya jiji,” alieleza Satura. - Aliongeza: “Hii itakuwa ni kanda na makao makuu yake yatakuwa ni Upanga Magharibi. Kwa hiyo kule tumepeleka wataalamu wa sekta zote na wananchi wa kanda hizo hawatalazimika kuja hapa kupanga foleni watahudumiwa kwenye kanda hiyo,” alifafanua. - Satura alisema kanda ya pili inahusisha kata za Gerezani, Ilala, Kariakoo, Jangwani, Mchikichini na Mchafukoge na makao makuu yatakuwa Gerezani. “Na hivi karibuni tunaenda kujenga ofisi kubwa zenye hadhi za halmashauri kwa hiyo hizi zitakuwa ni kama halmashauri ndogo,” alisema. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live