Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka ya Maji Igunga yadhibiti upotevu wa maji kwa asilimia 17.6

Picha Iguwasa Data Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga (Iguwasa), Humphrey Mmyombel

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga (Iguwasa) imefanikiwa kudhibiti tatizo la upotevu wa maji kutoka asilimia 26 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia asilimia 17.6 mwaka wa fedha 2022/2023.

Akizungumza na Mwananchi Julai 17, 2023, Mkurugenzi mtendaji wa Iguwasa, Humphrey Mmyombela amesema mafanikio hayo yamevuka lengo la awali la kupunguza upotevu wa maji hadi asilimia 24.

‘’Kiwango cha kawaida cha upotevu wa maji kinachoruhusiwa ni asilimia 20, sisi tumevuka hadi kufikia asilimia 17.6; haya ni mafanikio makubwa na tunakusudia kuendelea kudhibiti zaidi upotevu wa maji,’’ amesema Mmyombela

Ametaja ongeeko la idadi ya watumishi, hasa mafundi, kubadilisha miundombinu chakavu ikiwemo mabomba na dira za maji kuwa miongoni mwa siri ya mafanikio hayo.

‘’Kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, tumebadilisha dira chakavu 314 kwa kufunga mapya, hii imesaidia kuongeza mapato kwa kuhakikisha wateja wanalipa ankara sahihi kulingana na matumizi yao,’’ amesema .

Mtendaji mkuu huyo wa Iguwasa amesema mamlaka hiyo inakusudia kubadilisha miundombinu chakavu katika eneo lenye urefu wa kilometa tano, lengi likiwa ni kuhakikishia wateja huduma bora na kudhibiti zaidi upotevu wa maji.

Mkazi wa mtaa wa Hanihani mjini Igunga, Ibrahim Yassin aliupongeza uongozi wa Iguwasa kwa kushughulikia haraka taarifa za uharibifu wa miundombinu ya maji zinazotolewa na wateja.

"Nawashauri wananchi kuendelea kuisaidia Uguwasa kudhibiti siyo upotevu wa maji kwa kutoa taarifa za uharibifu katika maeneo yao,’’ amesshauri Yassin

Iguwasa ilianzishwa mwaka 1999 na kuanza kutoa huduma rasmi mwaka 2000. Mamlaka hiyo inayozalisha zaidi ya lita za ujazo milioni 4.1 za maji kwa siku inahudumia zaidi ya watu 123,625, sawa na asilimia 87.4 ya wakazi wa mjini wa Igunga na vijiji jirani.

Chanzo: Mwananchi