Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wajitokeza mazishi ya kaka yake Mbowe mkoani Kilimanjaro

69478 Pic+mbowe

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Mamia ya watu wamejitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Nshara Machame kushiriki misa ya mazishi ya Meja Jenerali mstaafu, Alfred Mbowe.

Alfred Mbowe alifariki dunia Jumapili Julai 28, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliagwa jijini Dar es Salaam Jumatano Julai 31, 2019 na  kusafirishwa kwa ajili ya mazishi yanayofanyika leo.

Mazishi ya Alfred ambaye ni kaka wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe yatafanyika katika kijiji cha  Nshara Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Viongozi mbalimbali wamefika katika kanisa hilo kushiriki misa hiyo itakayoanza saa 7 mchana.

Alizaliwa Januari 1953 na kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwaka 1973 na kustaafu utumishi jeshini mwaka 2009, akiwa amelitumia jeshi hilo miaka 36.

Chanzo: mwananchi.co.tz