Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wajitokeza kuwania maeneo ya biashara Dodoma

101662 Maeneo+pic Mamia wajitokeza kuwania maeneo ya biashara Dodoma

Wed, 8 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mamia ya wakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma nchini Tanzania leo Jumanne Aprili 7, 2020 wamejitokeza kuwania nafasi za kufanya biashara katika miradi miwili ya kimkakati iliyojengwa na Serikali.

Miradi hiyo ambayo itaanza kutoa huduma kabla ya Aprili 26, 2020 ni soko kuu la Ndugai na Stendi kuu ya mabasi.

Mwananchi limeshuhudia mamia ya wakazi wakiwa kwenye foleni katika viwanja vya ofisi ya jiji ya zamani.

Katika viwanja hivyo kulikuwa na maeneo matatu ambayo mtu analazimika kupita kabla ya kupata fomu hiyo ya biashara ambapo sehemu ya kwanza ilikuwa ni kuandika majina, kupata kuponi na kwenda kulipia.

Hata hivyo, kutokana na wingi wa watu baadhi ya watu walitakiwa kurudi kesho kwa ajili ya kuchukua fomu.

Akizungumza katika viwanja hivyo,  Beatrice David amesema amefika katika eneo hilo saa 2 asubuhi na kupewa fomu yake kwa ajili ya kuomba kiwanja kwenye stendi kuu ya mabasi ya Nzuguni.

Pia Soma

Advertisement
“Huyu baba amefanya vizuri sana kututangazia tuje kuomba. Na watu wamechangamkia fursa hii sana,” amesema.

Zoezi hilo lililoanza leo litamalizika Aprili 16, 2020 ambapo kila muombaji anatakiwa kulipia Sh20,000 ili kupata fomu ambazo hazitarudishwa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz