Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wajitokeza kushuhudia ma-DC wakila kiapo

Fri, 3 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi na watendaji mbalimbali wa wilaya za Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo na Kigamboni, Sara Msafiri Ally.

Hafla hiyo inayofanyika leo Ijumaa Agosti 3, 2018 itaongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pia atamkaribisha katibu tawala mpya wa mkoa huo, Abubakar Kunenge.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni wakuu wa idara kutoka wilaya za Kinondoni na Kigamboni, wakuu wa wilaya zote za Dar es Salaam, mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia na meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Wengine ni mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi  na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba.

 

Baada ya kuwaapisha viongozi hao, Makonda anatarajiwa kuzungumza na viongozi waliohudhuria hafla hiyo inayofanyika katika ukumbi wa Anatoglou.

Chanzo: mwananchi.co.tz