Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia waaga mwili wa kigogo wizara ya fedha

69397 Mwili+pic

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamia ya watu wamejitokeza katika Kanisa Katoliki Tabata Kinyerezi jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa ofisa mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe.

Lwajabe aliyekuwa mkurugenzi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini (EU) kupitia wizara hiyo, mwili wake ulikutwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani Julai 26, 2019 ukining’inia juu ya mti wa mwembe kwa mujibu wa familia yake.

Misa ya kuaga mwili wa  Lwajabe imefanyika leo mchana Agosti Mosi, 2019 na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali, wakiwemo mabalozi.

Mwili wa Lwajabe unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Ihembe, Karagwe mkoani Kagera  kwa mazishi yatakayofanyika Agosti 3, 2019.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz