Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambosasa aridhishwa kuona polisi wanachukua tahadhari na corona

4703 Kamanda Mambosasa Mambosasa aridhishwa kuona polisi wanachukua tahadhari na corona

Thu, 14 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP-Lazaro Mambosasa, amefanya ukaguzi wa vituo vya polisi jijini humo ili kuona namna vilivyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaoenezwa na kirusi aina ya corona.

Katika ukaguzi huo Kamanda Mambosasa ameridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Makamanda hao na jinsi wanavyoendelea kusimamia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya kwa kuweka ndoo za maji safi na sabuni, kuweka sanitazer na kuwa na vipima joto kwa ajili ya kupima wanaoingia katika vituo vyao.

Aidha, Kamanda Mambosasa amewataka askari na raia wanaofika vituoni kupata huduma kuendelea kuchukua taadhari dhidi ya maambukizi ya COVID 19 ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara na kutokaribiana (social distance) na kuepusha misongamano katika vituo vya polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live