Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo yaiva uwanja wa kisasa Dodoma

Fb88bec010a8e69f66cbf0289e9b5f11 Mambo yaiva uwanja wa kisasa Dodoma

Mon, 5 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amesema tayari michoro ya ujenzi wa uwanja mkubwa na wa kisasa jijini Dodoma imeshakamilika kilichobaki ni kutangaza zabuni ili ujenzi uanze mara moja.

Dk Abbasi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, na kusema serikali inaendelea na uboreshaji wa maeneo mbalimbali ya michezo ili kukidhi viwango vilivyowekwa kwa ajili ya mchezo husika.

Amesema tayari Uwanja wa Benjamin Mkapa umeshaboreshwa katika utekelezaji wa kazi hiyo, kwa kuwekewa bango lenye uwezo wa kuonekana mchana na usiku bila shida pamoja na kuwaasa mashabiki hasa wa mchezo wa soka kuwa wastaarabu hasa katika utunzaji wa miundombinu yake.

Pia amewataka wadau mbalimbali wa michezo kuwekeza katika ujenzi wa viwanja vya michezo na kutoa agizo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuendelea kusimamia ubora wa viwanja vya michezo wanavyovisimamia.

Katika hatua nyingine, Dk Abbasi amesema utaratibu wa kutumia N-Card unamsaidia mtumiaji kununua tiketi kupita simu ya mkononi kwa minajili ya kuzuia ujanja wa aina yoyote unaosababisha klabu kutopata mapato ya kutosha.

Chanzo: habarileo.co.tz