Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo ni 'super' miradi ya maji Morogoro

Kero Majipic Mambo ni 'super' miradi ya maji Morogoro

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amefanya ziara ya kikazi Mkoani Morogoro ambapo amekutana na viongozi pamoja na watumishi wa sekta ya mkoni humo.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu amepokea taarifa ya utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ikiwa ni pamoja na taarifa ya miradi, taarifa ya mwenendo wa hali ya maji katika mito na mabwawa pamoja na uchimbaji wa visima vya maji katika Mji wa Gairo.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hizo Kemikimba ameiagiza menejimenti ya Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kuhakikisha wanaendelea kutoa taarifa ya hali ya maji huku wakiainisha mahitaji ya maji kwa sekta mtambuka.

Aidha Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inajukumu la kuendelea kutafuta vyanzo vya maji kwa kufanya tafiti mbalimbali haswa kwenye maeneo ambayo hayana maji ili wananchi waendelee kupata huduma ya maji safi na salama.

Mbali na Hilo piaa amezitaka taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maji kuendelea kushirikiana kwa ukaribu katika kutekeleza majukumu yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live