Mamba mmoja anayesadikika kushambulia wananchi wa Kijiji cha Izindabo Kata ya Lugata Kisiwa cha Kome, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza amegeuzwa kitoweo na wananchi wa kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwagawia kitoweo hicho ambacho kitawapitia afya njema.
Damumbaya Majani moja wa wananchi waliochuna mamba huyo alishirikiana na Maofisa wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania (Tawiri) amesema;
"Nyama ya mamba ni lishe tosha na ni tiba mojawapo kwa magonjwa ya binadamu hasa wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo. Nyama ya mamba ina faida kubwa ndiyo maana wananchi wanaitamani kuitumia na nitiba pia inarutubisha mwili wa binadamu kiafya," amesema Majani.
Oparesheni ya vuna mamba inayofanywa na Maofisa wa Taasisi ya utafiti ya Wanyamapori (Tawiri) inalenga kuokoa maisha ya watu wanaofanya shughuri ndani ya Ziwa Victoria.
Wanyama aina ya mamba wamekuwa nitishio kwa wananchi wanaoishi kandokando mwa ziwa Victoria kutokana na kuwashambulia wakati wanapokwenda kuoga na kuteka maji na kufanya shughuri zingine za kibinadamu.
Kaimu ofisa Mtendaji Kijiji cha Izindabo Samweli Prospa ameongoza zoezi la wananchi wa Kijiji cha Izindabo kupata kitoweo hicho kwa kuzingatia ratiba walizojipangia kila.moja apate anayehitaji.
Mamba huyo amevunwa na Maofisa wa Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) kwa lengo la kuokoa maisha ya watu wanaoishi kando kando mwa ziwa Victoria.
Wananchi wamegawana nyama ya mamba baada kuvunwa huku ikisadikika mamba huyo ni miongoni mwa mamba wanaoshambulia wananchi wa Kijiji cha Izindabo na kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu.