Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama wa mwanafunzi aliyejinyonga apoteza fahamu akiaga mwili wa mwanae

16286 FAMILIA+PIC TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Amina Maro, mama mzazi  wa mwanafunzi  wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Rau mjini Moshi, Emmanuel Tarimo (18), aliyejinyonga hadi kufa, amepoteza fahamu wakati akiaga mwili wa mwanae.

Mwanafunzi huyo alijinyonga hadi kufa Septemba 4, 2018, saa chache baada ya kuhojiwa na jopo la walimu juu ya tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake.

Leo Jumamosi Septemba 8, 2018 ilifanyika ibada fupi ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, mama huyo baada ya kushuhudia mwili wa mwanae katika jeneza, alipoteza fahamu.

Watu mbalimbali leo wameaga mwili wa mwanafunzi huyo leo asubuhi katika mtaa wa Sabasaba kata ya Rau Wilaya ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro,   kuelekea katika kijijini cha Mashati Rombo kwa maziko.

Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alihojiwa na walimu wake kwa saa kadhaa akishinikizwa kukiri kufanya kitendo hicho, lakini aliwajibu kuwa hahusiki.

Soma zaidi

·VIDEO: Familia mwanafunzi aliyejinyonga yamgeukia mkuu wa shule

 

·VIDEO: Mwanafunzi ajinyonga baada kutuhumiwa kumpa mimba mwenzake

 

Chanzo: mwananchi.co.tz