Arusha. Hatimaye mama wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Ndeshikurwa Sikawa aliyekuwa amefungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kuomba Miriam Mrita ambaye ni mjane wa bilionea huyo kuondolewa kusimamia mirathi, amekubali kuondoa kesi hiyo ili kusaka maridhiano.
Uamuzi huo, umefikiwa Jumatatu, Octoba 21 2019, katika kikao cha kusaka suluhu katika mgogoro wa kugombea mali za bilionea huyo, baina ya watoto wake na ukoo wa Msuya kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.
Mama huyo alikuwa amefungua kesi hiyo namba 66 ya mwaka 2019 kuomba Mjane aondolewe na yeye kupewa jukumu hilo kwa madai ameshindwa kutimiza majukumu yake katika kugawa mali na akituhumu kuuzwa kwa baadhi ya mali.
Hata hivyo, mjane huyo kwa sasa yupo magereza akituhumiwa kwa kesi ya mauaji ya wifi yake Aneth Msuya ambaye aliuawa jijini Dar es Salaam.
Uamuzi wa kuondolewa shauri hilo ulitokana na maombi ya wakili wa Miriam na watoto wa Msuya.
“Upande wa Msuya wamefungua kesi hii mara ya tatu baada ya mbili kufutwa wakiomba kumuondoa msimamizi wa mirathi ambaye tayari alipitishwa na mahakama na wao kupokea mgao wa fedha zaidi ya Sh900 milioni,” alisema.
Habari zinazohusiana na hii
- Watoto wa bilionea Msuya hali bado tete
- VIDEO: Watoto wa bilionea Msuya wahofia kuporwa mali, waomba msaada
- VIDEO: Mtoto wa bilionea Msuya ashindwa kurejea kwenye nyumba ya baba yake, aitwa polisi