Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama na mwanaye wagundulika kufa ajali ya gari dogo, lori la Dangote

74257 Ajali+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vipimo vya Vinasaba (DNA) vimebaini maiti mbili za ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani Agosti 31, 2019 na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kukosekana kwa ndugu, ni ya mama na mwanaye.

Maiti hizo ni kati ya tano zilizopelekwa katika hospitali hiyo zikiwa zimeharibika kutokana na kuungua baada ya gari ndogo kugongana na lori la kampuni ya Dangote.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji,  Onesmo  Lyanga baada ya magari hayo kugongana lori hilo lilipoteza mwelekeo na kugonga nguzo ya umeme na nyaya kuanguka na kusababisha moto.

Amesema  gari dogo likiwa na watu wawili liliingia barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Mtwara bila kuzingatia sheria na kugongana na lori hilo lililokuwa na watu sita.

Septemba Mosi, 2019  MNH ilitoa wito kwa ndugu kujitokeza kupima DNA ili kutambua miili kabla ya kuzikwa ndipo walipojitokeza ndugu wa maiti tatu.

Waliotambuliwa ni Zahoro Gombo, Feruzi Sukari na Cadwell Msambwa ambao wote maiti zao zimeshachukuliwa kwa ajili ya mazishi.

Pia Soma

Advertisement
Ofisa uhusiano wa MNH, Sofia Mtakasimba ametoa kwa ndugu wa maiti mbili zilizosalia kujitokeza kwa ajili ya kipimo hicho cha utambuzi.

“Maiti tatu zimeshatambuliwa na kuchukuliwa zimebaki mbili li tunaomba ndugu  wajitokeze ili zoezi la kuwatambua lifanyike, kama una ndugu yako humuoni ni vyema ukaja ili kujiridhisha,” amesema.

Mkurugenzi wa Tiba shirikishi wa MNH, Dk Pracesa Ogweyo amesema wanahifadhi miili isiyo na ndugu kwa kati ya siku 14 hadi 21 kabla ya kuwakabidhi Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya maziko.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz