Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama na mtoto wafariki ajalini

Mauaji DRC Crime Scene Mama na mtoto wafariki ajalini

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki (mtoto wa miezi sita na mama mtu mzima) na wengine takribani 50 wamejeruhiwa katika ajali ya gari dogo  aina ya Tata liliokuwa linatoka Kigogo Freshi kuelekea Mloka kupitia Kisarawe baada ya kupinduka na kuingia kwenye Mto.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amebainisha hayo alipofika hospitali ya wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwapatia pole na kuwajulia hali majeruhi hao usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe disemba 19. 2023.

Adha akithibitisha kupokea majeruhi na miili ya waliofariki mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kisarawe Dkt.Risasi Rajabu amesema baadhi ya majeruhi waliopata majeraha madogo wamesha waruhusu na wengine wanaendelea kuwapatia huduma pamoja na saba wamewapatia rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa mwimbili. Ajali hiyo imetokea jana desemba 18 majira ya saa nane mchana.

Nae mkuu wa wilaya hiyo Fatma Nyangasa ameishukuru serikali kwa kuweza ujenzi wa vituo vya dharura ambavyo leo kimeweza kuokoa maisha ya watu na amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka itakapotolewa taarifa ya kitaalam kutoka katika jeshi la polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live