Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama mzazi wa Sugu afariki dunia

13970 SUGU+PIC TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mama mzazi wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Desderia Mbilinyi amefariki dunia leo Jumapili Agosti 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH).

Taarifa iliyotolewa leo na uongozi wa Muhimbili imesema, Desderia alikuwa amelazwa hospitalini hapo na hali yake ilibadilika usiku wa kuamkia leo na kuhamishiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).

“Mama mzazi wa Sugu (Mbunge) amefariki  leo  saa  3:00 asubuhi (akiwa) ICU,” imeeleza taarifa ya Muhimbili na kuongeza kuwa mwili umehifadhiwa hospitalini hapo.

Soma zaidi:Sugu asema afya ya mama yake itaamua lini ataibuka bungeni

Chanzo: mwananchi.co.tz