Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama, mtoto anayedaiwa kuwekwa kabatini waruhusiwa

37788 Pic+kabatini Mama, mtoto anayedaiwa kuwekwa kabatini waruhusiwa

Tue, 22 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Msichana aliyedai mwanaye kufungiwa kabatini kwa miezi mitano na mwajiri wake, wameruhusiwa kutoka hospitalini kwenda kuishi kambi ya kulea wazee na watoto ya Hombolo jijini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Januari 22, 2019, mkuu wa idara ya watoto Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma, Dk Muzzna Ujudi amesema Neema Matimbe (15) na mwanaye wamesharuhusiwa.

Naye ofisa ustawi wa jamii katika hospitali hiyo, Theresia Lawei amesemawawili hao wamepelekwa kwenye kituo cha kulelea wazee na watoto cha Hombolo.

“Baada ya kuona kurudi tena kwa bosi wake haiwezekani na hata kwa mama yake usalama unakuwa mdogo, tuliamua kuwapeleka kwenye kituo hicho kwa usalama zaidi huku utaratibu wa kupatiwa sehemu nzuri ya kuishi ukiendelea,” amesema Lawei.



Chanzo: mwananchi.co.tz