Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama amnyonga mtoto wake wa kumzaa

Crimeee Mama amnyonga mtoto wake wa kumzaa

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi Mkoani Mtwara linamshiklia mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Sinde Kata ya Msangamkuu, halmashauri ya Mtwara, kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na nusu.

Baadhi ya majirani wanasema mama huyo alimnyonga mtoto wake huku yeye na mtoto wakiwa uchi na kukimbilia porini ndio majirani walipomkimbiza na kumchukua mtoto lakini alikuwa tayari amefariki.

Kaimu Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live