Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama amdai mkwewe talaka ya binti yake

Talaka Mweee.jpeg Mama amdai mkwewe talaka ya binti yake

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mkwe, Rosemary Mayunga amemfikisha mahakamani mkwewe Godwin Mmbaga, akiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iamuru amchukue binti yake kwa ajili ya usimamizi na kumtunza kutokana na matatizo ya afya ya akili yanayomkabili.

Shauri hilo lilifunguliwa hivi karibuni na Rosemary akimtaka mwanawe Kuyega Mmbaga (48), kuwa chini ya uangalizi wake. Shauri hilo linasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Francis Mhina.

Rosemary katika madai yake anaiomba Mahakama itoe amri ya kuteuliwa kumsimamia Kuyega anayeishi katika ndoa maeneo ya Upanga, jijini Dar es Salaam anasumbuliwa na tatizo la afya ya akili.

Rosemary alidai kuwa yeye ni mama mzazi wa Kuyega Mmbaga na alimzaa mtoto huyo akiwa kwenye ndoa na mume wake Mayunga ambaye ameshafariki dunia.

Alidai mwaka 2002 Kuyega aliolewa na Mmbaga, wanaishi Upanga na walijaliwa kupata watoto watatu, lakini mmoja alifariki dunia na kubaki na watoto wawili.

Watoto waliobaki ni Kiminali Mmbaga (17) na Mariko Mmbaga (7).

"Mwanangu ni mfanyabiashara, yuko katika ndoa halali lakini maisha yake ya ndoa yametawaliwa na matatizo hakuna maelewano na mumewe Mmbaga hali inayosababisha Kuyega kuishi kwa mateso.

"Kuyega kila wakati anaumwa na kupona hali inayosababisha kushindwa kutekeleza majukumu yake, Julai 23, mwaka huu alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na ndugu yake na baada ya vipimo alibainika anaumwa.

"Katika uchunguzi alionekana ana matatizo makubwa ya akili yaliyodumu kwa miaka mitatu," alidai.

Mama huyo anadai sababu za kuomba amri ya Mahakama ni kutokana na matatizo yanayomkabili Kuyega ambaye mara kadhaa amekuwa akitaka kujiua.

Mwombaji aliambatanisha ripoti ya Dk. Frank Masao, ambaye ni Mkuu wa Kitengo Hospitali ya Taifa Muhimbili inayoonesha Kuyega anasumbuliwa na afya ya akili.

Alidai kwa tatizo alilokuwa nalo Kuyega, hawezi kutia saini nyaraka yoyote kisheria na tatizo lake kwa asilimia kubwa linachangiwa na mumewe Mmbaga.

Alidai kuwa Mmbaga amekuwa akimtishia kumuua kwa bastola mkewe na taarifa hizo waliziwasilisha Kituo Kikuu cha Polisi.

"Tulitoa taarifa Polisi kwa ajili ya usalama wa maisha ya Kuyega, askari alifika katika nyumba ya Mmbaga, alimkuta akataka kuchukua bastola yake, lakini Mmbaga alidai iko juu chumbani, kabla askari hajapandisha chumbani kuifata alimpekua na kumkuta nayo.

"Mmbaga alikamatwa na kupelekwa Polisi, mwanagu anapigwa, anadhalilishwa, anatishiwa bastola, ananyimwa uhuru wa kuchanganyika kwenye jamii.

"Amekuwa akimkataza kusoma Biblia badala yake anamlazimisha kusoma Kuran tukufu, kanisani haendi," alidai Rosemary katika hati yake ya madai.

Mahakama inatarajia kuanza kusikiliza shauri hilo Desemba 13, mwaka huu na mume (Mmbaga) anatakiwa ajibu madai yaliyoko dhidi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live