Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama aliyechora Tattoo ya mchungaji mwili mwake afunguka kila kitu

Mchungaji Tattoo Mama aliyechora Tattoo ya mchungaji mwili mwake afunguka kila kitu

Tue, 29 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja wa jijini Arusha, kwa jina la Elizabeth, aliyevuma kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni baada ya kuonekana amechora tattoo ya nabii mkuu GEORDAVIE, kisha kudai anampenda kupita maelezo amefunguka haya.

Elizabeth ambaye ni mama wa watoto watatu,amesema kuna taarifa zinazosambaa kwamba yeye yupo kwenye mahusiano na Nabii GEORDAVIE, amesema taarifa hizo siyo za kweli kwani yeye na nabii huyo hawana hata mawasiliano ya karibu isipokuwa ni nabii wake katika huduma za kimungu na kuwaomba watu waache kumchafua nabiii GEORDAVIE.

Alipoulizwa ni kwanini amechora tattoo ikiwa anajua kabisa vitabu vya dini vinakataza kuchora tattoo, amejitetea kwa kusema aliichora akiwa bado hajaokoka na hata baada ya kuokoka aliiona inaumuhimu mkubwa kwani kwake.

Amesema tattoo ya GEORDAVIE ni kama kinga inamsaidia sana akiwa kwenye shughuli zake za usiku, na hata kuna waumini wa dini wakubwa wamejichora tattoo kwa hivyo yeye haoni kama ni tatizo.

Elizabeth ameongeza kwa kusema yeye hajiwezi kabisa kwa nabii hiyo na hatajari watu watasema nini, atakuwa na nabii bega kwa bega licha ya watoto wake kutopendezwa na kitu anachokifanya lakini amesema yeye ndiye mama yao hivyo hawawezi kumpangia cha kufanya.

Aidha Elizabeth amemalizia kwa kusema mpenzi wake alimkimbia baada ya kuona anaelekeza mapenzi zaidi kwa nabii kuliko kwake, lakini yeye hakujali kwani nabiii GEORDAVIE kwake ni kama Mungu wa pili, hata hivyo baada ya tukio lile mwanamama huyo amesema aliondoka na kitita cha shilingi milioni moja na ameahidiwa milioni tano zingine kutoka kwa nabii huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live