Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama ajifungua ndani ya boti Zanzibar kwenda Dar

IMG 20230414 WA0175 Mama ajifungua ndani ya boti Zanzibar kwenda Dar

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Maryam Yahya Maulid mwenye umri wa miaka 25 leo, Aprili 14 saa 7:45 mchana amejifungua mtoto wa kiume akiwa ndani ya Boti ya MV Kilimanjaro V iliyokuwa ikitokea Zanzibar kwenda Dar es Salaam.

Mwanamke huyo amejifungua salama kwa msaada wa Daktari Suleiman wa Sealink na mtoto huyo amezaliwa na uzito wa kilogramu 2.5 na kupewa jina la Kilimanjaro V.

Akizungumza na Azam Online, mume wa mwanamke huyo, Isaka Musa amesema kwasasa mama na kichanga chake wanaendelea vizuri na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Temeke kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live