Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumkaba shingoni

Crime Scene 45.jpeg Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumkaba shingoni

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Mwananzige Dadi (34) mkazi wa Kijiji cha Sinde, Kata ya Msangamkuu Kwa kosa la kumuua mtoto wake (4) kwa kumkaba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa Disemba 12, 2022 saa nne usiku katika Kitongoji cha Ngw'ale Kijiji cha Sinde Dadi almkaba shingo mtoto wake hadi kusababisha kifo.

Amesema kuwa baada ya uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na daktari ilibainika kuwa chanzo cha kifo ni kukosa hewa baada ya kukabwa shingoni.

"Kwasababu tuko kwenye upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live