Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Samia azindua jengo la Sh1.8 bilioni Chuo cha Olmotonyi

26151 SAMIA TanzaniaWeb

Sat, 10 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu amezindua jengo la mihadhara la Chuo cha Misitu Olmotonyi cha jijini Arusha lenye thamani ya Sh1.8 bilioni.

Jengo hilo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 240 na bweni la wanafunzi 100 wa kike limejengwa kwa ufadhili wa Ufalme wa Norway ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuimarisha taasisi za elimu nchini ili zitoe elimu bora.

Majengo haya yatasaidia kupunguza uhaba wa madarasa na  adha kwa wanafunzi wanaoishi nje ya chuo. Tunaushukuru Ubalozi wa Norway kwa  kutoa ufadhili wa masomo katika ngazi ya astashahada na stashahada katika chuo hiki,” amesema Mama Samia.

Ubalozi wa Norway umetoa ufadhili kwa wanafunzi 128 wakiwamo wasichana 56. Unatekeleza mradi wa kujenga uwezo wa jamii kwa kuhamasisha usimamizi shirikishi wa misitu (Mkuhumi) na wa mabadiliko ya tabianchi maarufu kama ECOPRC.

Chuo cha Olmotonyi kimeunganishwa na mkongo wa Taifa na ufadhili kiliopata umewawezesha kuboresha maktaba   na kukiwezesha kununua vifaa mbalimbali vya kufundishia.

Ufadhili huu utasaidia kuimarisha mazingira na mafunzo yanayotolewa hivyo kukiwezesha chuo kuzalisha watalaam wenye ujuzi unaokidhi mahitaji,” amesema Mama Samia.

Awali, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alisema kutokana na uhaba wa mabweni chuo hicho kilikuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 600 wakati mahitaji halisi ni zaidi ya 1,000.

Lakini, uboreshwaji wa miundombinu uliofanywa utasaidia utoaji wa mafunzo ya kiwango cha juu.

Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jacobsen amesema  wananchi wajengewe uwezo ili wasikate miti ovyo baadala yake waongeze juhudi ya kupanda mingine.

Chuo cha Misitu-Olmotonyi  kilianzishwa mwaka 1937 kwa madhumuni ya kufundisha uhifadhi wa misitu na  kimekuwa tegemeo nchini na ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa ujumla.

Chanzo: mwananchi.co.tz