Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malupelupe wa Morogoro ayakanyaga kwa polisi

Moro690548862 Malupelupe wa Morogoro ayakanyaga kwa polisi

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mkoa wa Morogoro inamshikilia Emmanuel Charles maarufu kama Malupelupe (22) na enzake watano kwa kosa la wizi wa vitu mbalimbali ikiwemo Pikipiki, Simu janja na fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro, ACP Alex Mkama amesema watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 13, 2023 majira ya saa 4 usiku maeneo ya Miswala wakitumia Pikipiki aina ya Haojue yenye namba za usajili MC 270 DMS na walipora simu ndogo aina ya Tecno yenye thamani ya shilingi 30.000/- ne pesa taslimu shilingi 50,000/-.

Amesema, “mara baada ya kuwapekua walikutwa na Pikipiki mbili aina ya Haojue zenye namba za usajili MC 270 DMS na MC 414 CTW wanazotumia kufanya uhalifu, pia walikutwa na simu moja ndogo ainu ya tecno, makasha ya simu 13. pochi za kike 16 na simu janja 10 zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali.

Aidha, katika kusimamia sheria za usalama Barabarani jumla ya madereva 10 wa magari yanayo safirishwa nje ya nchi maarufu kama (IT) na ambayo hayajasajiliwa wamekamatwa wakiwa wamebeba abiria kinyume cha shera na wote walifikishwa Mahakamani kwa hatua za kesheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live