Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malori yakwama Makambako kwa zaidi ya siku 5

Malori Yakwama Makambako Kwa Zaidi Ya Siku 5 Malori yakwama Makambako kwa zaidi ya siku 5

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya malori 25 ambayo yanasafirisha bidhaa mbalimbali kutoka kiwanda cha karatasi Mgololo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa yamekwama kwa zaidi ya siku tano katika Kijiji cha Nyamande na Kitandiliko Halmashauri ya Mji wa Makambako Wilayani Njombe kutokana na ubovu wa barabara katika eneo hilo.

Madereva wa magari hayo wamesema changamoto kubwa katika eneo hilo ni Wakala wa barabara kuweka kifusi chenye tope na kusababisha magari kukwama hasa katika kipindi hiki ambacho mvua inanyesha na kuiomba Serikali kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami au changarawe kwani imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi.

Meneja wa TANROADs Mkoa wa Iringa Yudas Msangi amekiri kupokea changamoto hiyo na kueleza kuwa hali hiyo imesababishwa na mvua ambazo zinaendelea kunyesha na kusema wataifanyia marekebisho mvua zikipungua ambapo amesema mpango uliopo ni kuifanyia usanifu na kuiombea fedha ili ijengwa kwa kiwango cha lami kwa miaka ijayo.

“Lakini tutafanya tunavyoweza ili paweze kupitika na tunaenda kufanya upembuzi yakinifu ili baadaye huko fedha ikipatikana tuweze kujenga kwa kiwango cha lami lakini sio mpango wa leo au kesho”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live