Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malizeni miradi kwa wakati - RC Sendiga

Malizeni Miradi Kwa Wakati   RC Sendiga Malizeni miradi kwa wakati - RC Sendiga

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo Januari 23, 2024 amefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayoendelea katika mkoa wake wilayani Babati.

Ziara hiyo ilianzia katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) katika Hospitali ya Mji wa Babati, ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kujitahidi ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa haraka.

Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Mji Daktari Kyabaroti Kyabaroti amesema kuwa jengo hilo lilitengewa Mil. 300 ambapo mpaka sasa lipo katika hatua za umaliziaji na ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa Februari litaanza kutumika.

Jengo hilo la ghorafa nne ambapo likikamilika litakuwa na jumla ya vyumba vya ofisi 33 kati ya hivyo 06 ni vyumba vya ofisi za maafisa wakuu ngazi ya mkoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema utekelezaji unaoendelea ni awamu ya Kwanza ambayo ilianza baada ya Serikali kutoa fedha mnamo mwezi Aprili 2023 jumla ya shilingi milioni mia nane tu (TShs.800,000,000.00) ambazo zilipokelewa Polisi Mkoa Manyara.

Amesema kazi zilizofanyika ni ujenzi wa msingi, nguzo na sakafu za ghorofa zote nne huku wakifanya maandalizi ya ujenzi wa kuta za pamoja na kuezeka na ujenzi wa chumba cha mitambo ya lifti ambapo wanatarajia ujenzi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari.

Nae Mhe. Sendiga amewapongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kutekeleza mradi kwa vitendo huku akizitaka taasisi nyingine zenye miradi mkoani humo kuiga Jeshi la Polisi.

Aidha Mhe. Sendiga amemtaka mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kuhakikisha anasimamia kwa ufasaha ujenzi wa jengo la ofisi ya yake linakamilika kwa wakati maana ujenzi wake umekuwa ukisua sua jambo linaloleta ukakasi kila anapotembelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live