Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malezi ya Watoto: Wazazi tuwajibike – Dkt. Biteko

Screenshot 20231231 150346 Collage Maker GridArt Malezi ya Watoto: Wazazi tuwajibike – Dkt. Biteko

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amewataka wazazi nchini kuwajibika kuhusu malezi ya watoto ili kuepusha kuwa na kizazi kisichokuwa na maadili kujenga Taifa imara.

Dkt. Biteko ameyasema hayo jana Disemba 31, 2023, wakati akitoa salamu za mwisho wa mwaka kwenye ibada ya jumapili katika Kanisa Katoliki la Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Ushirombo wilayani Bukombe Mkoa wa Geita.

Amesema, wakati tukisherehekea Dominika ya familia, wazazi wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya kulea familia, na ndio maana hata mafundisho ya dini yameelekeza wajibu wa Baba, Mama, na Mtoto kwenye wajibu wa kila mmoja na kudumisha malezi ya familia na Upendo.

“Niwaombe wazazi tuwalee watoto kwenye maadili na kutimiza wajibu wetu ili kuepusha kuwa na kizazi cha walevi, majambazi kwani Jamii kwa sasa haiko vizuri” Alisisitiza Dkt. Biteko.

Akiwasilisha salamu za mwaka Mpya, Dkt. Biteko amewataka Watanzania na waumini kwa ujumla kumfanya japo mmoja kwenye Jamii kuwa mwenye furaha, kudumisha Upendo, Amani na kusisitiza kumuombea Mhe. Rais Samia na Serikali ili kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake, Paroko wa kanisa hilo Padri Julius Msobi, alimshukuru Biteko kwa kushiriki ibada hiyo ya misa Takatifu sanjari na jitihada anazozifanya kuhakikisha wananchi wa Bukombe wananufaika na Maendeleo na kumshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wa Bukombe.

Chanzo: Dar24