Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malecela ataja mambo mawili akiaga mwili wa Le Mutuz

Lemutuz 1 Pic Malecela ataja mambo mawili akiaga mwili wa Le Mutuz

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

John Malecela ambaye ni baba mzazi wa William 'Le Mutuz' amewaongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa mtoto wake huku akizungumza mambo mawili.

Le Mutuz ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malecela alifariki jana Mei 14, 2023 na leo ameagwa kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam na mwili wake kusafirishwa kwenda Dodoma kwa ajili ya mazishi yatakauyofanyika Jumatano.

Malecela, ambaye aliwaongoza waombolezaji kuaga mwili wa Le Mutuz, alitamka mambo mawili, akiwa ni mtu wa mwisho kuzungumza leo katika hafla hiyo.

"Nina mambo mawili ya kusema, ukoo wa Malecela tunataka kuwaahidi wote waliosema mema juu ya mwanangu (Le Mutuz) hapa tunayachukua kama nyota ya kutuongoza.

"Pili nawashukuru wote, mmetuvumilia, sina cha kuwapa ninamuomba Mwenyezi Mungu awajalie moyo mwema.

"Ndugu zangu, nikizidisha hapo nitakuwa sina uamini wa ninayo yasema," amesema Malecela kwa huzuni lakini alitoa sauti ya ukakamavu licha ya kuwa na umri wa miaka 89 sasa.

Awali mwenyekiti wa Kamati, Omary Kimbau alisema ratiba ya kuaga mwili wa Le Mutuz Dar es Salaam ni fupi na kwamba kubwa itafanyika Dodoma kesho na Jumatano kwenye maziko yake.

Waombolezaji walianza kuaga mwili wa Le Mutuz saa 7:05 mchana, ikiwa ni baada ya salamu za rambirambi, kusomwa wosia wa marehemu, neno la shukrani la familia, viongozi wa Serikali na marafiki zilizoanza mara baada ya mwili kuwasili saa 5:24 asubuhi katika viwanja vya Karimjee.

Omary amesema baada ya kifo cha Le Mutuz, Malecela (baba wa Le mutuz) jana alisema anakuja Dar es Salaam kuupitia mwili wa kijana wake akitokea Moshi na kwenda Dodoma kwenye mazishi.

"Sisi tulikuwa na wazo rafiki yetu apumzishwe hapa Dar es Salaam na ndugu zake wa hapa, Mzee akasema anakwenda kuzika Dodoma, alituruhusu tumuage ndugu yetu leo kabla ya kwenda Dodoma, lakini hata hili angeweza kukataa," amesema.

Katibu wa kamati, Sebastian amesema aliwasiliana na Le Mutuz saa chache kabla ya kifo chake.

"Aliniuliza uko wapi? nikamwambia nyumbani, asubuhi napata taarifa amefariki, lakini nilichojifunza kwake ni uvumilivu, alikuwa haonyeshi kama ni mtu mwenye shida, wakati mwingine anapost picha au video lakini sura yake haionyeshi kama yupo kitandani," amesema Mzee Malecela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live