Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malalamiko ya wavuvi kufanyiwa kazi

793f7bdbe74f6c5242846f7b4f324166 Malalamiko ya wavuvi kufanyiwa kazi

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, amemtaka Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Rashid Tamatama kuhakikisha anakamilisha utafi ti wa malalamiko ya kanuni ya mwaka 2020 ambao umekuwa ukifanywa na Taasisi ya Utafi ti wa Uvuvi Tanzania(TAFIRI) kabla ya Machi 23.

Akizungumza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Paulina Gekul alisema kanuni hizo za mwaka 2020 zimekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wavuvi kuhusu mita 50 za bahari, uvuvi wa nyavu mtando na kutaka kazi hiyo ikamilike haraka kabla ya Machi 23.

Gekul alimtaka katibu mkuu huyo kuhakikisha wavuvi wote ambao hawajashirikishwa wanashirikishwa ipasavyo. Alieleza kuwa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa marekebisho ya kanuni za uvuvi za mwaka 2020 serikali imeazimia kuzipitia upya ili ziendane na mahitaji ya sasa.

Alisema hivi karibuni wizara imepokea maoni na changamoto mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya uvuvi kutoka Ukanda wa Bahari, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria kuhusiana na marekebisho ya kanuni ya uvuvi ya mwaka 2020 katika baadhi ya vipengele.

Gekul alisema maeneo ambayo yameonesha kuwa na changamoto nyingi ni katika uvuvi wa kutumia nyavu za mtando wakati wa mchana katika ukanda wa Bahari ya Hindi, utaratibu wa kupima ukubwa wa macho ya nyavu kwa kutumia kipimo kilichoainishwa katika kanuni kinachofahamika kama Mesh Gauge na uvuvi wa dagaa wakati wa mbalamwezi.

Kutokana na changamoto hizo, Waziri wa Mifugo, Mashimba Ndaki hivi karibuni alitoa maelekezo kuwa TAFIRI ifanye utafiti kuhusu uvuvi wa kutumia nyavu za mtando na hivyo inatakiwa kutoa majibu kabla ya Machi 23.

Aidha Gekul alisema wizara haifurahishwi sana kuwa na msururu wa makatibu wakuu wa vyama vya wavuvi.

“Kuna katibu Mkuu Uvuvi, Dar es Salaam, Katibu Mkuu Uvuvi ziwa Victoria, Katibu Mkuu Ziwa Tanganyika, Katibu Mkuu kila mahali, nakuagiza Kaitbu mkuu wa wizara yetu Tamatama lisimamie hili haraka sana kuhakikisha mnawaunganisha wote na kuwa na chama kimoja.

Chanzo: www.habarileo.co.tz