Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makubwa! Mbaroni kwa kumbaka mbuzi jike

Mbuzi Ehk.jpeg Makubwa! Mbaroni kwa kumbaka mbuzi jike

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Patrick Mgimba anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 - 26, Mkazi wa Kijiji cha Boimanda Halmashauri ya Mji wa Njombe anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumnajisi mbuzi jike aliyekuwa amefungwa kamba kwenye eneo la malisho ya kijiji.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Boimanda, Anatory Mligo, amesema Mgimba amefanya tukio hilo October 6, 2022 majira ya mchana wakati akitoka shambani kwake na kuwaomba vijana wawili wachungaji wa mifugo wasitoe siri yake kwa ahadi ya kuwapa Sh. 25,000 ambapo baadaye alishindwa kuwalipa.

“Huyu Kijana alitoka shambani sasa pale kulikuwa na vijana waliokuwa wanachunga na mifugo huwa ina hali ya kutawanyika sasa vijana wakati wameenda kurudisha mifugo ambao walikuwa wanaenda nje na eneo la machungio ndipo yeye akaona baadhi ya mbuzi waliokuwa wamefungwa kamba hawana wenyewe na kufanya kitendo hicho” amesema Mtendaji huyo.

Mligo amesema Mtuhumiwa amekamatwa kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa vijana hao wawili walioshindwa kukaa kimya na kufikishwa katika kituo kidogo cha Polisi kilichopo kata ya Uwemba pamoja mbuzi aliyefanyiwa kitendo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live