Mwenge wa uhuru umeingia Mkoani Manyara ukitokea Kilimanjaro na unatarajia kukagua, kutembelea, kuona na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 29 yenye thamani ya sh6.6 Bilioni.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere, akizungumza mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakati akipokea mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai, amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa Kilomita 1,089.3.
Makongoro amesema Mwenge huo utaweka mawe ya msingi ya miradi 10 ya thamani ya sh3.7 Bilioni na kuzindua miradi minne ya thamani ya sh342.3 milioni.
Amesema utafungua miradi mitatu ya thamani ya sh534.3 milioni na kukagua na kuona miradi 12 ya thamani ya sh2 bilioni.
“Mwenge wa uhuru utakimbizwa kwenye tano za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang’ na Mbulu, kisha kuukabidhi mkoa wa Arusha Juni 16,” Makongoro.
WANAFUNZI WAJENGEWA UWEZO KUFANYA MAAMUZI, KUJIEPUKA NA VISHAWISHI KIPINDI CHA LIKIZO