Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda kupima wanaume tezi dume

6859 MAKONDA RC TZW

Sun, 22 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ana mkakati wa kuanza kupita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuwapima wanaume saratani ya tezi dume baada ya kukamilika kwa shughuli ya utoaji chanjo kwa ajili ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa miaka 14.

Utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi jijini hapa unatarajiwa kuanza Aprili 23 huku wasichana 24,087wakitarajiwa kupata chanjo hiyo.

Makonda ametoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa uliowakutanisha Wakuu wa Idara, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Waandishi wa Habari, Viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini ili kuzungumza kuhusu utoaji wa chanjo hiyo.

Alisema wataalamu mbalimbali wamekuwa wakizungumzia sana saratani ya mlango wa kizazi ambayo huathiri wanawake lakini wameisahau tezi dume ambayo inaumiza zaidi akina baba huku mwamko ukiwa mdogo kulizungumzia suala hilo.

Ameongeza kuwa, wanaume pia wamekuwa hawapimi wakihofia upimaji uliokuwa unatumika awali na kusema kuwa kwa sasa wataalamu wamekaa na kuja na kipimo ambacho ni tofauti na awali.

"Wengi wamekuwa na kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa njia zetu zile jamani kwa sasa siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi, hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu kuhakikisha hii kasi ya vifo kwa kinababa inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu," alisema Makonda.

Chanzo: habarileo.co.tz