Wed, 9 Oct 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ametoa rai kwa viongozi mbalimbali wa serikali mkoani mkaoni Arusha kuhakikisha ya kwamba hakuna mfanyabiashara yeyote anayeonewa au kunyanyasika mkoani humo
Makonda amewaasa viongozi hao kuwa waadilifu na kutenda haki kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha huku akibainisha kuwa kiongozi yeyote atakayeonea wafanyabiashara kibarua chake kitaota nyasi
Makonda amebainisha kuwa lengo la serikali ya awamu ya 6 ni kuhakikisha kila mfanyabiashara anafanya biashara kwa uhuru na amani na kwa kufuata sheria za nchi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live