Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda awashangaa wapinzani kuhoji demokrasia, bomoabomoa

32433 Makondapic Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Unaweza kusema kauli aliyoitoa mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam iliyofanyika eneo la Kimara Stop Over imemshangaza  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kauli hiyo ya Mnyika imemfanya Makonda kuwashangaa wabunge wa upinzani wanaokosoa jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Makonda ameyaeleza hayo  leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika  hafla hiyo baada ya Mnyika aliyepewa nafasi ya kusalimu wananchi na kugusia suala la demokrasia, kutaka waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi huo kulipwa fidia na kudai kuwa wananchi mtaani vyuma vimekaza.

Baada ya Mnyika kumaliza kuzungumza, Makonda amesema anashangazwa na mbunge huyo kutaka wananchi walipwe fidia badala ya kusifia mradi huo.

Amesema licha ya jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli bado kuna watu wanampinga, huku akitolea mfano elimu bila malipo na ununuzi wa ndege.

“Mnamhukumu kuwapatia fedha, mnamhukumu kwa kupanua barabara nane ili msipate tabu ya usafiri. Hivi  mnapokaa nyie na akili zenu mnawaza nini, na mbaya zaidi hata ofisi zao pale makao makuu wameshindwa

kuzitengeneza,” amesema Makonda.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz