Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda awapa siri wanaotaka vyeo

53082 Pic+makonda

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar. Watumishi wa Serikali wanaotaka kupanda vyeo wametakiwa kuacha majungu, uzembe na fitina na badala yake wafanye kazi kwa weledi na ufanisi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema hayo jana wakati ilipokuwa akikagua ujenzi wa ujenzi wa ghorofa 12 za Magereza Ukonga.

Alisema ziara yake hiyo ni muendelezo wa ukaguzi wa miradi yote inayofanyika mkoa wa Dar es Salaam. “Nikiwa mkuu wa mkoa nawajibika kufuatilia miradi yote inayofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam kwani inatekelezwa chini ya Rais na wanufaika ni wananchi hivyo napaswa kujua hali ilivyo na kuona pale ambapo mkoa unaweza kuongeza chachu ili spidi iongezeke,” alisema.

Makonda alisema mradi huo ulikuwa ukiendeshwa na TBA lakini kutokana na kusuasua Rais John Magufuli alipoutembelea Machi 16 mwaka huu alitoa maelekezo kwa Jeshi la Wananchi Tanzania kuuchukuwa ili ukamilike kwa wakati.

Msimamizi wa ujenzi wa majengo hayo, Brigedia Mbuge alisema kati ya ghorofa hizo, nane zitakuwa za askari, nane za maofisa.

Alisema wanaoshiriki ujenzi huo maofisa wa jeshi, askari, vijana na wafungwa 33 ambao waliomba kufanya shughuli ndogondogo.

Alisema awali ujenzi huo ungekamilishwa na TBA zingekaa familia za askari 320, lakini sasa zitakaa familia za askari 172 na kwamba fedha zilizotolewa zilikuwa za ujenzi wa ghorofa nne.



Chanzo: mwananchi.co.tz