Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda awaonya makandarasi kuhusu Rushwa

54846 Pic+makonda

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda amewataka makandarasi kuacha tabia ya kusaka tenda kwa kutoa rushwa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 30 katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi ya elimu, afya , maji na barabara  aliyoifanya  kuanza Aprili 13 hadi 24 katika halmashauri zote za jijini Dar es Salaam.

Amesema kutokana na kuwapo hali hiyo, ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwafuatilia makandarasi wote wanaofanya kazi katika mkoa huo ili kuwabaini wanaofanya vitendo vua rushwa.

"Rushwa ni adui wa haki, hakikisheni mnapata kazi kwa kufuata vigezo vinavyohitajika,“ amesema.

Hata hivyo, Makonda ameupongeza mkoa wa Dar es Salaam kwa kuongoza katika ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha robo mwaka ambapo takwimu zinaonyesha umekusanya zaidi ya Sh118.4 bilioni, ikifuatiwa na  Dodoma ambao umekusanya Sh 57.3 bilion, huku Mwanza ukikusanya Sh 22.9 bilioni.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kwa sasa makusanyo kwa mkoa wa Dar es Salaam yapo vizuri hivyo kuanza sasa hakuna kibali kutolewa kwa maofisa wanaohusika na makusanyo ya  mapato wakiwamo wakurugenzi kwenda nje ya mkoa huo kujifunza.

Amewataka wataalamu kuweka mfumo mizuri ya ukusanyaji wa mapato ili mkoa wa Dar es Salaam ufikie asilimia 100 badala ya asilimia 73 iliyopata katika kipindi hicho.



Chanzo: mwananchi.co.tz