Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda awamilikisha maeneo wafanyabiashara Kimara

21908 BIASHARA+PIC TanzaniaWeb

Fri, 12 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Kimara-Mwisho wamejimilikisha maeneo ya biashara baada ya kupewa ruksa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Wafanyabiashara hao walikuwa wakiuza bidhaa pembezoni mwa hifadhi ya barabara baada ya eneo la mwanzo kufungwa kwa ajili ya huduma ya kupaki magari.

"Leo ni siku ya Alhamisi, siku ya Jumamosi nitamtuma mkuu wa wilaya hapa na aliyepata tenda eneo hili. Siku ya Jumamosi wafanyabiashara mtaanza kufanya biashara hapa mpaka tutakapopata eneo la kudumu," amesema.

Wakizungumza leo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika eneo hilo, walieleza kuwa wamekosa eneo la kufanyia biashara baada ya Tanroads kufunga eneo hilo.

Makonda aliagiza kufunguliwa kwa eneo hilo na ifikapo Jumamosi waanze kufanya baishara zao jambo lililowafanya kuanza kugawana maeneo dakika chache baadaye.

Emmanuel Manoni amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa eneo kwa ajili ya biashara zao huku akisema uamuzi huo ni ahueni kwao.

"Hili eneo tulikuwa tunafanyia biashara na baadaye mmiliki alifunga kwa ajili ya Parking (eneo la kuhifadhia magari) tukahamia barabarani,"amesema.

Ramadhani Said amesema kupewa eneo hilo kutaondoa adha ya kufanyia biashara barabarani.

"Sisi tunamshukuru mkuu wa mkoa kwa kutoa eneo hili kwa sababu tuliondolewa na lilikuwa halitumiki," amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz