Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda awaapisha wajumbe wa mabaraza ya ardhi Dar

Makonda awaapisha wajumbe wa mabaraza ya ardhi Dar

Sat, 23 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaapisha wajumbe saba wa mabaraza ya ardhi Wilaya ya Kinondoni na Temeke.

Makonda amefanya hivyo kulingana na matakwa ya Sheria ya Ardhi inayomuagiza ashirikiane na waziri mwenye dhamana kuwateua wajumbe hao na baadaye kuwaapisha.

Walioapishwa  leo Jumamosi  Novemba 23, 2019 ni Petro Mukani, Balozi Celestine Liundi, Manana Mlunde, Denik Murusuri, Sikunjema Yahya, Rutami Chisumo na Fatuma Chikundo.

Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe hao,  Makonda amesema anatarajia kuona wanafanya kazi kwa makini na kupunguza migogoro ya ardhi.

"Msibaki kutumia nyaraka na makaratasi  zinaweza kuwanyima haki watu nendeni mkatende haki, Dar es Salaam ni Jiji la wajanja watu wanaweza kukosa haki," amesema Makonda.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe waliahidi kwenda kutenda haki na kutumia busara katika kumshauri mwenyekiti wa baraza wa wilaya katika kufikia maamuzi ya utatuzi wa migogoro.

"Wananchi wawe na amani kwa sababu busara na hekima vitasaidie tumshauri vizuri mwenyekiti, nawaahidi tutasimamia sheria kufanya kazi hii," alisema Sikunjema Yahya kutoka Temeke.

Chanzo: mwananchi.co.tz