Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda aunda kamati ya watu 15 Dar

24837 Pic+konda TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameunda kamati ya watu 15 kwa ajili ya kupambana na watu wanaojihusisha na biashara ya ngono.

Amesema baadhi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wamempigia simu na kumuomba awasaidie kuondokana na hali hiyo kwa sababu wamechoshwa nayo.

Ameyasema hayo leo Oktoba 31, 2018 wakati akitangaza kamati hiyo iliyoundwa kwa ajili ya kupambana na vitendo hivyo pamoja na wanaotapeli wengine kwa kutumia mitandao wakijifanya ni viongozi maarufu nchini.

Makonda amesema wapo baadhi ya watu wanaoingizwa katika dimbwi hilo bila kupenda huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya ambayo hawawezi kuimudu.

Amesema kwa sababu wapo baadhi ya watu walioingia katika dimbwi hilo kwa kubakwa na kudanganywa wameongeza watu wa ushauri nasaha ili waweze kuwasaidia kimawazo ili waweze kuondokana na suala hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz