Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda atoa saa 24 wabunge walioko Dar es salaam kuondoka

1177 Makonda 660x394.png Makonda atoa saa 24 wabunge walioko Dar es salaam kuondoka

Wed, 6 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam kuhakikisha wanarudi Bungeni, tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

Makonda amesema kuwa Mbunge anayepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye kibali au ruhusa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tofauti na hapo ni vyema wakarudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Mbunge anayepaswa kuwepo Dar es Salaam ni yule mwenye kibali cha Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, asiyekuwa na kibali huyo ni mzururaji kama wazururaji wengine," - amesema Makonda

"'Hatujaalika wazururaji kutoka mikoani, inawezekana wakahatarisha zaidi maisha ya wakazi wa Dar es salaam kwa kuwaambukiza corona, kipindi hiki ni muhimu katika Bunge la Bajeti dhidi ya mahitaji ya wananchi" ameongeza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live