Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda atimiza ahadi Simba, amkabidha Manula Sh10mil

61143 Pic+makonda

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametimiza ahadi yake kwa kuwakabidhi wachezaji wa Simba waliofanya vizuri msimu huu Sh 24 Milioni.

Mbali na wachezaji, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara katika fedha hizo alipata mgao wa Sh3 Milioni.

Makonda amesema utaratibu huo hautaishia kwa Simba ataendelea kufanya kwa wanamichezo wengine watakaofanya vizuri Dar es Salaam

Mkuu huyo wa mkoa alitoa fedha hizo kwa kipa Aishi Manula aliyepewa Sh10 Milioni.

Manara aliyepewa Sh3 Milioni, mchezaji wa Simba Queens, Mwanahamisi aliyepewa Sh2 Milioni.

Wengine kwenye mgao wa fedha hizo ni beki Erasto Nyoni, kiungo James Kotei, mshambuliaji John  Bocco, mchezaji chipukizi Rashid Juma, Medie Kagere na Chama.

Pia Soma

Nahodha wa Simba, John Bocco alimshukuru Makonda kwa motisha hiyo akisisitiza kuwa Simba itaendelea kufanya vizuri.

Simba msimu huu imetetea ubingwa wake wa Ligi Kuu na kujihakikishia kwa mara nyingine kushiriki Ligi ya mabingwa Afrika.

Chanzo: mwananchi.co.tz