Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda atangaza kuzisajili ndoa zote Dar, wanaume walaghai kukiona

71005 Pic+makonda

Tue, 13 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda amesema kuna mpango wa kuanzisha kanzi data ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.

Kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa.

Makonda amesema pamoja na kanzidata hiyo atatumia mkutano wa SADC kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanawake kuumizwa hivyo wakati umefika wa kuanza kushughulikia.

“Tutaanza kuangalia na kupata uzoefu kwa wenzetu wa SADC ambao kama haya wanashughulikiaje na mkutano ukiisha tutajadiliana kama mkoa tunawezeshaje usajili huo,” amesema

“Kanzidata hii itawasaidia wanawake wasitapeliwe, mtu akitaka kukuoa utaenda mtandaoni na kuangalia taarifa zake, utabaini kama ameoa au la na vilevile itawasaidia hata wanawake ambao wameolewa ili kuzuia waume zao wasioe kwa siri,” ameongeza

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz