Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda ataka viongozi kuiga mazuri ya Bujugo

23592 Makonda+pic TanzaniaWeb

Wed, 24 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka viongozi kuishi kwa kuwatendea mema watu wote kama ilivyokuwa kwa marehemu Julian Bujugo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 23, 2018 wakati akiongoza waombolezaji katika ibada ya mazishi ya Bujugo aliyekuwa diwani wa Magomeni (CCM) na mmiliki wa  shule za Green Acres.

Bujugo alifariki dunia Oktoba 18, 2018 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Massana iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Makonda amesema Bujugo alikuwa akisimamia haki kwa kuwatetea wanyonge hasa kunapokuwa na mgogoro.

"Tunatakiwa kuishi na kuwatendea mema watu wote kama alivyofanya marehemu Bujugo enzi za uhai wake," amesema Makonda.

"Kulikuwa na mgogoro mkubwa baina ya marehemu na wananchi katika eneo lake alikuja kwangu na  tukalimaliza.”

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Chongolo amesema marehemu alikuwa ni mdau wa elimu kwa muda mrefu hivyo tasnia ya elimu imepata pigo.

"Nimefahamiana na marehemu kwa muda mrefu kutokana na kazi alizokuwa akizifanya hasa kwenye tasnia ya elimu alikuwa ni mdau mkubwa sana," amesema Chongolo.

Chanzo: mwananchi.co.tz