Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza Sh165 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara za Mkoa huo katika bajeti ya 2019/2020 zitumike kama zilivyopangwa.
Ameeleza hayo leo Jumatatu Februari 24, 2020 wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, akibainisha kuwa barabara zote zilizoharibika kwa sababu ya mvua zinapaswa kurekebishwa.
"Barabara zote zisizopitika pesa hizo zipitike kikarabati miundombinu, acheni kasumba ya pesa kutengwa lakini haitumiki ipasavyo. Pesa zitafutwe na ziende kuboresha miundombinu ili barabara zipitike,” amesema.
Makonda amesema Mkoa wa Dar es Salaam una mtandao wa kilomita 5,153 za barabara kati ya hizo 1,300 ni za lami, 1,170 za changarawe na 2,979 za udongo.
Amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kusimamia miundombinu ya barabara kwa kutoruhusu wananchi kutupa taka hovyo.
"Mamlaka za mitaa zilinde miundo mbinu zisiendelee kuwatazama watu wanaoharibu na kutupa taka hovyo. Utupaji wa taka ndio unaofanya mitaro izibe na kusababisha mafuriko," amesema Makonda.
Pia Soma
- VIDEO: Dk Mashinji awasili mahakamani, Halima Mdee akataa kumsalimia
- Maneno ya Mama Samia yanawafaa sana wapinzani Uchaguzi 2020
- VIDEO: KAKA WA TUNDU LISSU ASEMA MAZITO KUHUSU KESI YA LISSU
"Nguzo za Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) hazijaondolewa na hii inafanya mkandarasi asuesue kufanya kazi kulingana na mkataba," amesema Kumbilamoto.