Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda apiga marufuku magari ya Utalii kusimamishwa

WhatsApp Image 2022 05 10 At 11.jpeg Makonda apiga marufuku magari ya Utalii kusimamishwa

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kutokukamata magari ya Utalii kwenye Mkoa wa Arusha na badala yake ukaguzi kwa Watalii ufanyike kwenye mipaka na kwenye viwanja vya ndege vinavyotumika na Watalii.

Makonda ameyasema haya mbele ya Waandishi wa habari June 08, 2024 kwenye Viwanja vya Magereza Kisongo kwenye maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Karibu Kili Fair 2024, yanayojumuisha Makampuni zaidi ya 700 ya kimataifa kutoka kwenye mataifa zaidi ya 50.

"Kama Serikali ya Mkoa tumeona tuweke mazingira bora zaidi ya kuhakikisha kwamba Mtalii anapokuja kwenye mkoa wetu hapati changamoto na ajisikie kuheshimika kwa sababu Taifa limejiandaa kupokea Watalii, kuanzia tarehe moja mwezi wa saba tumekubaliana kwamba hakuna Polisi kusimamisha gari la Utalii”

“Hakuna kusimamisha gari lililobeba Watalii kutoka Airport au Namanga kuingia katikakati ya Mji wa Arusha, tunafanya hivyo tukifahamu ya kwamba Watalii hawa wanakuwa wamekaguliwa katika Airport au mipaka, hawana sababu yoyote ya kuwekewa vikwazo viwili vitatu vinne mpaka saba wanasimama barabarani na kupoteza muda wao" RC Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live