Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Makonda amtaja Amber Rutty kuongezeka kwa joto Dar’

31809 Ambertupic TanzaniaWeb

Sat, 15 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji hilo kutumia mitandao ya kijamii kusambaza vivutio vya utalii na sio picha zenye maudhui ya ngono.

Makonda ametoa wito huo leo Jumamosi Desemba 15, 2018  wakati wa uzinduzi wa chaneli ya utalii inayofahamika kama Tanzania Safari Channel.

“Tutumie mitandao kutangaza utalii sio mambo ya Kiamberutty ambayo yanasababisha joto kuongezeka katika jiji letu.”

Makonda ametumia pia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kutenga muda wao kwa ajili ya kumuomba Mungu apunguze joto lililokithiri huku akieleza kuwa miti imeanza kukauka.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ameendelea kumwagia sifa Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita kwa kile anachodai kuwa anaunga mkono maendeleo.

 “Natambua uwepo wa meya wa jiji naomba usimame watu wakuone unavyounga mkono maendeleo,”

Soma Zaidi: Amber Rutty ashtakiwa kwa kucheza picha za ngono, akosa dhamana

Hii si mara ya kwanza kwa Makonda kumsifia Mwita  ambaye ni diwani wa Chadema kutokana na mwenendo wake wa kufanya kazi na viongozi wa Serikali bila kujali tofauti za vyama.

Soma Zaidi: Amber Rutty apata dhamana baada ya kusota siku 25 mahabusu



Chanzo: mwananchi.co.tz