Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekwepa kuzungumzia kuziwa kuingia nchini Marekani kwa maelezo kuwa kuna siku atalizungumzia suala hilo.
Makonda ametoa majibu hayo leo Ijumaa Februari 14, 2020 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, kutaka kutoulizwa masuala binafsi.
Februari Mosi, 2020 Marekani ilieleza kumzuia Makonda kuingia Marekani pamoja na mkewe, Mary Massenge na kwamba sababu ni tuhuma za kushiriki kukandamiza haki za binadamu.
Pia Soma
- Makonda ataka kukutanishwa na ‘wanaokesha’ wakibishana mitandaoni
- Mtanzania anayedai anaweza kutibu virusi vya corona matatani
- TRA wakamata bidhaa za mamilioni kutoka Kenya
Katika kipindi hicho ambacho Makonda alikuwa anazungumzia mambo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam, aliulizwa kama tayari ameshapokea barua kutoka Marekani ya kumpiga marufuku kuingia nchini humo.
Akijibu sali hilo, Makonda amesema kuwa leo alifika katika kipindi hicho kuzungumzia masuala ya kiserikali si binafsi.
“Hapa nimekuja kama mkuu wa mkoa, subiri nikija binafsi tutajadiliana, nimekuja kama Serikali,” amesema
Amewataka watangazaji wa kipindi hicho, Babbie Kabaye na Hassan Ngoma kumtafuta wakati mwingine ambapo ataweza kuzungumza kuhusu masuala yanayomhusu yeye binafsi.