Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda aahidi Sh120 milioni kugharamia matibabu ya watoto

63900 Jkcipic

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) nchini Tanzania imepokea hundi ya Sh20 milioni kutoka taasisi ya Jamal Patel kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 10.

Watoto hao ambao upasuaji wao unaanza keshokutwa Jumatatu Juni 24, 2019 ni wale watokao familia duni ambao wazazi wao hawawezi kumudu gharama za matibabu wakitokea mikoa mbalimbali.

Akizungumza leo Jumamosi Juni 22, 2019 wa kukabidhi hundi hiyo Mwenyekiti wa ukoo wa Patel, Harish Patel amesema mbali na msaada huo jitihada zaidi zinahitajika kuelimisha jamii juu ya tatizo la moyo.

“Mara nyingi tatizo la moyo hugundulika baadaye ambapo wazazi wameshatumia gharama kubwa kwa kutajiwa magonjwa mengine hii inatokana na kukosekana wataalamu wakutosha katika vituo vya afya hasa vijijini wa kugundua dalili za awali za ugonjwa wa moyo,” amesema Harish

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kuwalipia gharama za upasuaji wa moyo watoto kumi kila mwezi kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2019.

Amesema msaada huo utalenga watoto kutoka mikoa yote ya Tanzania wanaotoka familia masikini.

Pia Soma

Hivyo Makonda atalipia watoto 60 kutoka Julai hadi Desemba ambapo atatoa jumla ya Sh120 milioni kwa kumlipia kila mtoto Sh2 milioni

“Kwa hiyo mtanipa idadi ya watoto hao mwishoni mwa mwezi huu lengo ni kurejesha furaha kwa baba na mama ambao wamepoteza furaha kwa kukosa Sh2 milioni za matibabu kwa watoto wao, lakini pia kuokoa maisha ya watoto hao ambao ndiyo viongozi wajao,” amesema mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema tatizo la moyo bado ni kubwa hivyo msaada zaidi unahitajika ili kufanikisha matibabu kwa wagonjwa.

Amesema katika watoto 100 wanaozaliwa kila siku mtoto mmoja ana tatizo la moyo.

“Hapa tulipo tuna watoto 500 ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji na mbaya zaidi tunapokea kutoka mikoa mbalimbali kwa hiyo idadi hii inaweza kuongezeka,” amesongeza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz