Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda aagiza kampuni ya Nyanza kutopewa zabuni nyingine

16787 Pic+makonda TanzaniaWeb

Tue, 11 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameiagiza kampuni ya Nyanza kutopewa kazi nyingine hadi watakapomaliza miradi waliyoianza.

Kampuni hiyo ina miradi mitatu katika Manispaa ya Temeke ikiwamo barabara ya Chang'ombe yenye urefu wa kilomita moja.

Hayo yameelezwa leo Septemba 11  wakati akikagua miradi ya ujenzi wa barabara za halmashauri ya Temeke.

Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 15 lakini hadi sasa ni miezi 11 haijafika hata asilimia 25 ya ujenzi.

"Mkataba uliosainiwa ni wa miezi 15 hadi sasa ni miezi 11 mradi unasuasu hata asilimia 25 ya ujenzi bado" amesema Makonda na kuongeza:

"Ninaagiza kwa halmashauri zote kampuni hii ya Nyanza isipewe kazi yoyote kwenye Mkoa wangu hadi watakapokamilisha miradi mitatu waliyoianza.”

Mkurgenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa kusuasua na hivyo amewataka wajitathmini kwa kwani hawatapata tena zabuni kwenye Halmashauri hiyo.

"Nilipofika Temeke niliwaambia kwenye halmashauri yangu ujanja ujanja hakuna hivyo wajitafakari kwa kina kwani nnaweza kuvunja mkataba," amesema

Kwa upande wa meneja mradi wa kampuni ya Nyanza Noeli Nkinga amesema changamoto waliyokutana nayo ni pamoja ucheleweshwaji wa bomba lililotakiwa kuhamishwa.

"Tulitakiwa tumalize ndani ya miezi 15 lakini tumechelewa kutokana na bomba lililotakiwa kuhamishwa ambapo halikuhamishwa kwa wakati," amesema Nkinga.

Chanzo: mwananchi.co.tz