Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Washukuruni wanaowabania

33099 Makonda+pic Tanzania Web Photo

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mtu yeyote aliyekubania katika maisha unapaswa kumshukuru badala ya kumlaumu kwa kuwa amekuwa moja ya mafanikio yako.

Makonda aliyasema hayo usiku wa Jumamosi Desemba 22, 2018 kuamkia Jumapili  aliposhiriki katika tamasha la Tigo-Fiesta lililofanyika viwanjani vya Posta jijini Dar es Salaam.

Akitolea mfano, Makonda amesema wapo watu walionyanyaswa na ndugu zao wakiwemo shangazi na walezi lakini leo wana maisha mazuri na wengine wameweza hadi kujilipia kwenda fiesta.

Katika usiku huu, Makonda aliutumia kumuombea Ruge ambaye amelazwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu.

Wakati akipanda jukwani Makonda ambaye alikuwa amevalia nguo nyeusi iliyofunika sehemu kubwa ya kichwa chake ndani akiwa katanguliza fulana nyeupe iliyobana mwili wake, amesema Ruge anapaswa kuombewa na kila mtu kwa kuwa hakuna asiyejua mchango wake katika tasnia ya muziki na vijana kwa jumla.

Ni kutokana na hilo, aliamuru kusimamishwa wimbo wa piga makofi wa Profesa Jay aliokuwa kawekewa kabla ya kuanza kuzungumza na kurudiwa kwa clip inayomuonyesha Ruge akiwa anaelezea ndoto zake za kuuinua muziki wa Tanzania.

Baada ya kumalizika aliagiza umati uliohudhuria tamasha hilo, kila mtu kukaa kimya kumuombea Ruge.

Katika maombezi hayo aliyoyaongoza mwenyewe ya kuomba Mungu amrudishe Ruge nchini akiwa na hali nzuri ya kiafya watu walikuwa wakiitikia amina mpaka pale alipomaliza.



Chanzo: mwananchi.co.tz